Mshabiki wa G.Unit kabla ya kuenjoy albam yao baadae mwaka huu wataenjoy mixtape kwanza kabla ya albam kutoka kundi hilo liloungana wiki chache zilizopita na kuachia ngoma inayoitwa They talked about Jesus, 50 cent aliongelea albam na mixtape wakati akipiga stories na Hot 93.7 na Jenny Boom Boom.
Kuhusu filamu ya BMF alisema hakutakiwa kuwaomba memba wa G.Unit kufanya kwa sababu tayari wana haki ya kufanya.
Akizungumza repa huyo kutoka Queens, albam ya G.Unit itatoka Novemba au Desemba mwaka huu ikianza mixtape, Pia alifunguka kuhusu ishu kuwahusu G.
Unit nakusema kitu chochote kuhusu G.Unit yote yanaelekezwa kwake na sio Lloyd Banks, Tony Yayo au Young Buck. 50 cent aliyasema hayo kupitia video iliyopostiwa youtube na Hot New Hip Hop.com
Kati ya project nyingine za filamu imepangwa kufanywa ya Black Mafia Family (BMF) na hiyo ni moja ya filamu 10 ambazo amewekeza mkwanja
“Ilikuwa ni project ambayo tumeletewa na Lionsgate na Barry na Stan, waliongea na sisi kuhusu hili nikasema nilifanya kwa hiyo nafanya BMF pamoja na kuhakikisha inafanyika fresh na haki zote kuhusu filamu hiyo ziko tayari, kwa sababu fungu lake lilikuwa limeshaunganishwa na hicho ndicho nachokifanya, nilikusanya dola milioni 200, tukagawa kwenye picha 10 na tukauza haki zote kwa Lionsgate” alisema 50 cent.
Akiongelea mixtape na studio albam kutoka kwa G.Unit ikiwa ni surprise baada ya wiki chache baada ya kuungana tena kwa kundi hilo ingawa watu wamesema mengi miezi michache iliyopita, 50 cent aliperform na Tony Yayo, Lloyd Banks na Young Buck wakati wa show ya Music Festival.