George Kavishe Meneja Wa Bia Ya KilimanjaroKatibu Mkuu Mtendaji baraza La sanaa la Taifa BASATA Geofrey Ngereza Akielezea Historia Ya KTMA mbele ya waandishi wa Habari
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tuzo za kilimanjaro Tanzania Music Awards Zilizofanyika katika ukumbi wa mikutano Hotel Ya Kebbys iliyopo Bamaga Jijini DaR es Salaam, George Kavishe Amesema Kutokana na kutaka kuboresha zaidi Tunzo Hizo kwa mwaka huu wamekaa na kuchanganua na kuamua kafunya mabadiliko kadhaa ikiwemo yale ya kuwashirikisha wananchi kwanza katika swala zima la uchaguzi wa Nyimbo au wasanii ambao wao watapenda wawepo katika vipengele vinavyoshindwaniwa katika tuzo hizo kwa kupendekeza kupitia website Maalum Ambayo Itatangazwa pia kupitia njia ya sms Fina Mango Mkurugenzi OnePlus Communication ambao ni moja ya waratibu wa tuzo hizo akifafanua Jambo
Kavishe aliongeza kuwa Ile Academy iliyokuwa inafanya kazi hiyo kwa miaka ya nyuma itaendelea kuwepo ili kufanya uhakiki wa nyimbo na wasanii waliopendekezwa kuwa ni wa mwaka husika na kama wapo kwenye vipengele sahihi
Mtangazaji wa PlanetBongo Eatv & Radio Abdallah Ambua Dullah akiuliza Swali
Katika mabadiliko mengine yaliotajwa na mratibu Wa Tuzo Hizo kutoka Basata Ndg:Meregesi Ng’oko Kulwijira Amesema kuwa kipengele cha Mtayarishaji chipukizi kimetolewa kwasababu hakileti maana, ya kwamba chipukizi mtayarishaji bado hajaibuka kwahiyo haiwezekani kushindanisha hicho kipengele na zaidi ya hapo majina hujirudia kila mwaka
Waandishi kutoka vyombo mbali mbali vya habari katika Hafla Ya Uzinduzi Huo
Pamoja na hayo pia mabadiliko mengine ni pamoja na neno MSANII limeondolewa na kuwekwa MTUMBUIZAJI na MMUIMBAJI katika vipengele vilivyokua vinahusisha Msanii kwa sababu zilizoelezwa kuwa Msanii Lina simama Katika Maana Nyingi
Mengine ni video bora ya muziki ya mwaka badala ya video bora ya wimbo, neno muziki lina uwanja mpana kuliko wimbo pia tutakua na wimbo bora wa Afropop badala ya wimbo bora wa bongopop, kutakua na wimbo bora wenye vionjo vya asili ya kitanzania badala ya wimbo bora wenye vionjo vya asili’
Msanii bora chipukizi anaeibukia badala ya msanii bora anaechipukia…. wapo wasanii wengi sana chipukizi huko mtaani na miziki yao haijasikika, inawezekana amekaa miaka mingi akifanya kazi zake lakini akaibuka na ameonekana’
Somoe Ng’itu Kutoka Gazeti La Nipashe akifurahia jambo na muandishi Mwenzake wakati wa Uzinduzi wa tuzo za kilimanjaro Tanzania Music Awards 2014
Kwa hivyo tuzo za mwaka huu zitakua na jumla ya Vipendele 36 huku 34 tu ndio vitakavyopigiwa Kura na Watanzani, Vile Viwili ni uteuzi kutoka Basata kwajinsi watakavyoona wao nani wanastahili katika vile vipengele vya mtu au taasisi iliyochangia kuufanya muziki wa Tanzania kuendele vizuri