Wakiwa wameshinda tuzo ya AFRIMMA nchini Nigeria kama Best African Group & Producer of The Year kundi la Sauti sol kutoka nchini Kenya hatimaye wameonyesha cover ya albamu yao inayotegemea kutoka siku si nyingi, zikiwemo ngoma zinazopatikana ndani ya albamu hiyo ikiwa ni tatu inayoitwa “Live and Die in Africa”.
Sauti Sol walionyesha mashabiki zao kwa picha tofauti tofauti ambazo zilikuwa hazieleweki wanamaanisha nini hatinaye wakaja wakapost cover artwork ya albamu hiyo ya Live and Die in Africa.
Cover ya albamu hiyo imepigiwa African Heritage House, imekuwa kivutio kwa watu wengi na kushika headlines mbali mbali katika vyombo vya habari kwa jinsi walivyoonekana kwenye cover hiyo.
Cover artwork hiyo imetengenezwa na celebrity stylist Annabel Onyango.
Katika cover hiyo ya alabmau ya “Live and Die in Africa”, Sauti Sol na aina utamaduni wao inaonyesha uhalisia na kufurahia Uafrika.