Kushoto ni picha hiyo iliyomponza na kulia ndio mwanamke mwenyewe akiwa na mwanae
Mama mwenye watoto wanne amefungiwa ukurasa wake wa instagram baada kupost picha ya mtoto wake baada ya kuvunja sheria za mtandao huo kwa kuonyesha kifua cha mtoto wake mwenye miezi 19, mama huyo alikuwa na Followers 40,000 wanaomfuata katika mtandao wake kabla ukurasa wake haujafungwa.
Mama huyo analalamika kwa kufungiwa mtandao wake kwa sababu mtoto wake ni mdodgo wala picha hiyo haina ubaya wowote, Instagram wao wameona kama ni vibaya lakini wa mama wengi wamekuwa wakipost picha za watoto wao wakiwa wamevaa nepi lakini hawakusema ni vibaya lakini ya mtoto wangu Instagarm wameona sio sawa.
Mama huyo anasema Yule ni mtoto tu alidhani ni picha nzuri kupost kwa ajili ya mtoto huyo akionyesha tumbo lake huku akifurahia.
Hakuna kitu kibaya lakini hayo ndo yamemkuta mama huyo kwa hiyo wale wote mnaotumia instagram muangalie picha zipi za kupost yasije yakawakuta yaliyomkuta mama aliyepost picha ya mtoto wake wa miezi 19.