Kampuni inayotengeneza simu marufu ya Iphone Apple imekanusha kuwa simu zao za Iphone 6 zinajipinda
Kupitia kwa taarifa kampuni hiyo imesema kuwa simu zilizojipinda ni nadra sana kwa sababu wametumia vifaa dhabiti na zenye kudumu kuzitengeza.
Aidha apple imesema kuwa simu 9 pekee ndizo zimeripotiwa kujipinda na kuwa wenye simu hizo watapewa simu zingine mpya.
Apple imesema kuwa inaendelea kutathmini ubora wa bidhaa zake na kusema kuwa simu hizo Iphone 6 na Iphone 6 zilipassi majaribio kadha ya kutathmini ubora wao.
Taarifa hiyo imetolewa baada ya shinikizo kutoka kwa wateja wa kampuni hiyo ambao kwa usaidizi wa makampuni pinzani yamekuwa yakiendesha kampeini ya kunadi bidhaa zao ambazo bila shaka zimepata pigo kubwa kufuatia kuzinduliwa kwa simu hiyo ya Iphone 6 na Iphone 6plus juma lililopita.
Tayari takwimu zinaonesha kuwa simu milioni 10 tayari zimeuzwa kati8ka kipindi cha siku tatu tu tangu kuzinduliwa.
Awali ,Watu kadhaa ambao ni watumiaji wa iPhone 6 wamekuwa wakituma picha zao kwenye mtandao wa MacRumors ambazo zineonekana kuonyesha simu zao zikiwa na tatizo hilo.
Mwandishi wa habari kwenye mtandao wa ‘Geek.com’ pia aliripoti kuwa simu yake ye iPhone 6 imejipinda.
Na haijulikani nini hasa kinachoifanya simu hiyo kujipinda, baadhi wakisema huenda ni gamba lake ambalo limetengezwa kwa madini ya Aluminium ambalo linaifanya rahisi kwa simu hiyo kujipinda.
Taarifa za iPhone 6 kujipinda hazijaripotiwa tu kwenye blogu za habari za kiteknolojia bali pia kwenye vyombo vya habari kama Independent, the Washington Post, India Today na the Sydney Morning Herald.
Russell Holly, anayefanyia kazi mtandao wa habari wa geek.com,ni mmoja wa wale walioripoti kuwa simu yake imejipinda.
Watumiaji wa mtandao wa kijamii wa Twitter, wametu moani yao kuhusu habari za simu hiyo kujipinda.
Kampuni ya Apple ilipoulizwa kuhusu ripoti hizo lakini haijasema chochote mpaka sasa.
Mmoja wa wataalamu wa maswala ya kiteknolojia, anasema kuwa kampuni ya Apple inapaswa kuchunguza malalamiko hayo na hata kutoa taarifa rasmi haraka iwezekanavyo.
Jasdeep Badyal anasema kuwa Apple inapaswa kujibu madai hayo na kisha ikiwa ni kweli, basi inapaswa kuchukua hatua ya kuwapa simu mpya watu walioripoti kuwa simu zao zimejipinda.
Aliongeza kuwa hata kama kulikuwa na simu kdhaa tu zenye tatizo hilo, kampuni hiyo inapaswa kutoa taarifa na kueleza kilichofanyika.
(By BBC Swahili).