
Mwanasheria wa Meek Mill anasema kwamba maombi mawili ya dharura ya kusikilizwa kesi ya Meek Mill yamekataliwa, kwa hiyo imeonekana kwamba repa huyo kutoka Philladelphia atabaki jela mpaka Septemba.
Taarifa kupitia Philly.com ziliripoti kwamba maombi ya dharura ya mwanasheria wa Meek Mill Christopher Warren ya kusikilzwa tena kwa kesi hiyo yalikataliwa na jaji aliyemhukumu repa huyo.
Warren leo Jumatatu 21 amepanga kuandika barua kwenda mahakama ya juu zaidi akisema jaji Genece Brinkley aliyemuhukumu Meek Mill, anazuia kusikilizwa kwa maombi ya dharura kwa ajili ya hukumu ya Meek Mill.
Meek Mill alikamatwa mapema mwezi huu kwa kile kilichoripotiwa kwamba alivunja masharti aliyokuwa amepewa baada ya kupost picha kwenye ukurasa wake wa instagram akiwa ameshika silaha, akawa amevunja masharti aliyokuwa amepewa kutokana na makosa yake ya mwanzo (Probation violation) ndipo akafungwa jela kati ya miezi mitatu hadi sita.
