Taarifa kupitia TMZ zinasema Bwana wa mwamitindo anahusika na Deal Or No Deal amejiua kwa kujipiga risasi wiki chache baada ya kuona picha mke wake akila uroda na muigizaji Leornado DiCaprio na Adrian Grenier.
Picha Za Utata Za Katie akiwa na Leornado DiCaprio
Vyombo vya kisheria vimeiambia TMZ Andrew Stern alijipiga risasi kichwani Jumapili wakati akiwa katika eneo la kushoot huko San Femando Valley. Stern mwenye miaka 40 akiwa ni mfanyabiashara alikuwa amemuoa Katie ambae alikuwa mshiriki wa Americas Next Top Model.
Katie alipigwa picha huko Cannes mwezi uliopita na Leo na walionekana katika hali kimahaba. Pia kuna picha nyingine zikimuonesha Katie akiwa Cannes na Adrian Grenier iliripotiwa na TMZ. Katie na Leo Cannes na Adrieb huko Los Angeles.
Habari zinasema wamehojiwa watu tofauti tofauti baada ya kujiua akiwemo Katie mwenyewe walisema vitu vilivyokuwa vikimsumbua Andrew ni msongo wa mawazo uliosababishwa na masuala ya ndoa. Taarifa zaidi zinasema kwamba, Katie baada ya mahojiano alisema walikuwa katika mchakato wa kupeana talaka kati yake na Andrew.
Model Katie
Mtu mmoja karibu na Leo alisema kwamba Leo na Katie na muigizaji huyo hawakuwa pamoja na waliondoka club na GF wake Toni Garm. Kwa kuongeza kwenye suala la matatizo ya ndoa, Andrew alikuwa na historia ya msongo wa mawazo na masuala ya kibiashara