Aliyekuwa boyfriend wa mtoto wa Bobby Brown, marehemu Bobbi Kristina, Nick Gordon amemuomba Bobby Brown amruhusu ahudhurie maziko ya Bobbi Kristina siku ya kesho Jumamosi. Taarifa za TMZ zimeeleza kwamba Nick anaomba sana aruhusiwe aweze kuhudhuria maziko ya Kriss, ametuma barua pepe kwa Bobby Brown akiomba amruhusu.
Barua pepe iliyoonekana kutoka kwa Nick kwenda Bobby Brown inasema
“I loved Krissi with all my heart and I am destroyed that she is gone and I need to say goodbye.””I’m begging you both to please put your differences aside and allow me this chance.” “Krissi loved me very much and she would want me there.”
Katika barua pepe hiyo alimtaja Pat Houston ambaye ndiye anayeandaa maziko hayo
Bobby Brown wamekuwa hawaelewani na Nick Gordon kwa sababu amekuwa akilaumiwa na familia ya Whitney Houston kutokana na kifo cha Kriss na hata aliondoka kwenye mazishi mapema kutokana na kutoelewana kwa viti vilivyokuwa vimeandaliwa watu wakae.
Bobbi Kristina alifariki siku ya Jumatatu 27/07/2015 baada ya kukaa hospitali kwa miezi 6 toka Januari 31 mwaka huu.
Bobbi Kristina alikutwa ameanguka bafuni uso ukiwavumezama kwenye maji kwenye bathtub, akiwa hajijui kuanzia alikimbizwa hospitali akawa akitumia mashine inayomfanya aweze kuishi mpaka juzi Jumatatu ilipotangazwa amefariki.
May her soul rest at peace…..Amen