Nyambizi inayofanya shughuli ya utafutaji wa ndege nambari MH370 ya Malaysia iliyopotea mwezi mmoja uliopita, imezama kwenye kina kirefu katika jitihada za kutafuta mabaki ya ndege hiyo. Nyambizi hiyo Bluefin 21 imepiga mbizi kwenye kina kirefu zaidi katika eneo la utafutaji wa ndege hiyo baharini, baada ya nyambizi ya awali kushindwa kufika kina hicho.
Timu ya wafutaji imetumwa kwenye Bluefin 21 iliyo bahari ya Hindi jana ambapo itafanya zoezi la utafutaji wa ndege hiyo kwenye ardhi ya bahari, baada ya kushindwa kwa siku sita kupata ‘signals’ zilizoaminika kuwa zilikuwa zinatoka kwenye kisanduku cheusi cha ndege hiyo.
Mamlaka zinazosimamia utafutaji huo zinatambua kwamba mabaki ya ndege hiyo, MH370 inawezekana yako kwenye ardhi ya bahari na nyambizi hiyo, Bluefin 21, ina uwezo wa kufika umbali huo. Watafutaji wa ndege hiyo bado wanaamini kwamba mabaki ya ndege hiyo yanaweza kupatikana, licha ya kipindi kirefu kupita.