
Habari njema kwa wapenda burudani wote Afrika Mashariki, Nani hamjui Rabbit aka Kaka Sungura? Au nani hamjui Rich Mavoko? Kama huwajui, toka porini uje uanze kuishi na watu wanajua mambo yanayoendelea mjini.
Rabbit na Rich Mavoko ni majina mawili makubwa sana katika kiwanda cha muziki wa Afrika Mashariki na muziki wao ni mkali na hakuna wa kuuzuia au kuwa na maswali yasiyokuwa na msingi.
Ngoma kali “Ligi Soo” na “Roho Yangu” kwa njia moja ni ngoma ambazo umewafanya wasanii hao kufanya vizuri katika muziki wa Afrika Mashariki.
Habari nzuri kwa wawili hao kwenye colabo hiyo, unategemea nini kutoka kwa wakali hao kupitia hiyo colabo?
Habari hizo ziliwekwa wazi na Rich Mavoko mwenyewe kupitia instagram yake, ndipo alipopost cover ya single hiyo.
