Kibongo bongo ukianza kutaja maproducers ingawa wameibuka wengine kibao siku za karibuni, huwezi kuacha kumtaja P.Funk, Master J, Enrico, Marko Chali, Q The Don, Dunga, Mika Mwamba, Ludigo na list ndeeefu inaendelea.
Green Label nchini Marekani imewamulika maproducers wakali kwa miaka 10 iliyopita ambao wameendelea kuilea hip hop bila kupoteza utamaduni wake kwa miaka 10. Katika list hiyo yupo Dr. Dre, Dj Premier, J.Dilla, Mannie Fresh.
Unaweza usimalize kutaja list ya maproducers wakali katika gemu la hip hop kwa sasa na miaka 10 iliyopita, Green-Label.com katika list hiyo pia wamemtaja Kanye West na Just Blaze ambao wote wanamchango mkubwa katika ngoma kali za Jay Z ya The Blue Print album ambayo wengi wameisifiakuwa na beats kali.
Nje ya Just Blaze na Kanye West katika list hiyo yupo Rick Rubin. Jay Z alikuwa smart sana na kumchukua mkali huyo na kutengeneza hit ya 99 Problems katika albamu ya The Black Album, Green Label pia wamemsifia Rick Rubin kwa mchango wake mkubwa wa ubunifu katika album ya Magana Carta Holy Grail, pia amefanya Yeezus ya Kanye West na album ya mwisho ya Eminem ya The Marshal Mathers 2.
Hadi hapo unaweza ukaona uwezo wa maproducers waliotajwa na Green Label, wametengeneza ngoma ambazo mpaka sasa hivi ukisikia unaipenda Hip Hop na kuifanya iendelee kuishi ingawa kuna miziki kibao inafanya vizuri lakini Hip Hop inabaki pale pale kuwa great music kutokana na maproducers hawa.