Wiki hii mkali Boss Taylor Gang Wiz Khalifa ameshika namba moja kwenye chart za Billboard katika Top 200 albums chart na albamu yake ya Blacc Hollywood, wakati huo huo Iggy Azalea ameendelea kutesa na The New Classic na kuelekea mafanikio kama Beyonce amepanda hadi namba 45 na self-tittle project.
Wiz Khalifa ametua namba 1 na Blacc Hollywood
Wiz Khalifa na albamu yake ya Blacc Hollywood wiki hii ipo namba 1, na imeuza copies 90,453 wiki ya kwanza ilipoanza kupatikana, Sio albamu tu ya Wiz Khalifa ndo ipo kwenye chart ipo Statik Selektah amefungua wiki hii na What Goes Around, albamu ambayo imekamata namba 77 na imeuza copies 3,818 katika wiki yake ya kwanza, Albamu ya Slaine inayoitwa King of Everything Else nayo imekamata chart katika nafsi ya 189 na imeuza copies 1,954 katika wiki ya kwanza.
IGGY AZALEA ANAENDELE KUFANIKIWA NA ALBAMU YA THE NEW CLASSIC
Iggy Azalea na albamu ya The New Classic imerudi kwenye top 15 wiki hii, albamu ya repa huyo imeuza copies 12, 438 wiki hii, imeshuka asilimia 5 ukilinganisha na wiki iliyopita ambapo iluza copies 13,135, lakini yote kwa yote albamu yake imepanda kutoka nafasi ya 17 hadi nafasi ya 14 ikiwa ina wiki 18 toka ilipotoka, Jumla mpaka sasa imeuza copies 308,442 toka ilipoingia sokoni.
Beyonce amepanda mpaka nafasi ya 44 na Self-titled Album Beyonce
Albamu ya Beyonce self titled albam imerudi kwenye top 45 wiki hii, muimbaji huyo ambae aligonga vichwa habari kwenye MTV VMA na video ya vanguard award na performance yake wikiendi iliyoisha , amepanda kutoka nafasi ya 88 hadi 44 na self titled albam yake ambayo ilitoka wiki 37 zilizopita mwezi Desemba 2013. Albam hiyo iliuza copies 5,515 wiki hii, imefanya vizuri kwa asilimia 63 katika mauzo ukilinganisha na wiki iliyopita iliuza copies 3,392 na mpaka sasa imeuza copies 2,039,835.
Mauzo ya albamu kwa wiki moja kuanzia tarehe 24/8/2014.
#1. Wiz Khalifa – Blacc Hollywood – toka imetoka imeuza copies 90,453 (90,453)
#14. Iggy Azalea – The New Classic – wiki hii imeuza 12,438 na mpaka sasa imeuza 308,442.
#25. Trey Songz – Trigga – wiki hii imeuza 9,398 na mpaka sasa imeuza copies 222,638l.
#32. Linkin Park – The Hunting Party – wiki hii imeuza 6,880 na mpaka sasa imeuza copies 221,286).
#39. Tank – Stronger – wiki hii imeuza 6,151 mpaka sasa imeuza copies 22,772.
#44. Beyonce – Beyonce – wiki hii imeuza 95,515 na mpaka sasa hivi 2,039,835.
#45. John Legend – Love In The Future – wiki hii imeuza 5,494 na mpaka sasa imeuza copies 606,392.
#49. Eminem – The Marshall Mathers LP 2 – wiki hii imeuza 5,319 na mpaka sasa imeuza copies 134,580.
#52. Pharrell – G I R L – wiki ya kwanza imeuza copies 5,177 na mpaka sasa imeuza copies 506,919.
#58. August Alsina – Testimony – wiki ya kwanza imeuza copies 4,642 na mpaka sasa imeuza 188,418.