Mwigizaji na mwanaharakati wa maswala ya haki za Binadamu, Bibie Angelina Jolie pamoja na Waziri wa Mambo ya Nnje wa Uingereza, William Hague wamefanya ziara katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kujitazamia na kujaribu kuangalia njia za kufanya ili kupunguza na kuondoa kabisa vitendo vya ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia.
Kwa mujibu wa mtandao wa France 24, Jolie alitembelea kambi iliyopo huko kaskazini Magharibi mwa Goma ili kujionea uhalisia na uelewa wa vitendo hivi ubakaji katika ukanda huo ambao umekuwa na vita.Katika ziara hii, Hague amesema kuwa, Matumizi ya nguvu kingono katika mgogoro yanaweza kutatuliwa tu endapo migogoro hii itaanza kutatuliwa kwanza.
Translate Credit Sammisago.com