
Ukikubalika na repa kama Eminem basi wewe ni noma na inadhihirisha kwamba zile stories za siku za nyuma zilizosababisha maneno mengi baada ya Kendrick Lamar kuonekana kama ndo King of New York basi inaweza ikawa kweli kwa sababu mkali anayewakilisha Detroit Eminem kumkubali sana songstress wa wimbo wa Swimming pool.
Kuna hasira fulani unaweza ukahisi kuhusu Kendrick Lamar anarap kuwa repa bora duniani, ni repa mshindani na hicho ndo kitu ambacho kitaongoza maisha yake na hatapotea kwa muda mrefu atakuwa katika gemu.
“Kiroho safi nakubali anachokifanya Kendrick Lamar na ukweli yuko kwenye camp moja, yuko Aftermath, hicho tu kinasababisha awepo The Marshall Mathers LP2, alikuja Detroit, tukatisha kwa dakika chache, unajua na nilihisi mzuka jinsi alivyo na kila kitu, yuko fresh sana na mpole, wakati tukifanya ngoma na nadhani hiyo ilikuwa ni wiki moja au mbili kabla hajafanya vesi kwenye ngoma ya control” alisema Eminem.
“Kama pembe yangu sio kali, pia upanga wangu sio mkali, na sitaki kupambana na mtu mwingine ambae upanga wake sio mkali, Ukipata chuma mbili ambazo sio kali zikawa zinasuguana unadhani nini kitatokea hapo? Zote zitakwenda kuwa kali, kila mtu ambae yuko kwenye kiwanda hiki wamepoteza pembe zao, Hakuna chuki kweli, unatakiwa useme vitu tofauti na kila kitu ni kilaini” alisema Kendrick Lamar.
Ambae kwa sasa ni repa anaeshika headlines kibao unapotaka kuongelea gemu la Hip Hop duniani.
